Matumizi ya Mbinu ya Weusi na Uwili: Tathmini ya Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea (Dkt. Dorcas Muendi Musyimi Chuo Kikuu cha Chuka)

Sale!

KSh5,000.00

Category:

Description

IKISIRI
Kulingana na Wamitila (2008), matumizi ya mtindo katika kazi za fasihi ndicho kipengele ambacho humtofautisha mtunzi mmoja na mwingine. Hii inatokana na ukweli kwamba kila mtunzi anao mtindo wake wa kuwasilisha jambo mbele ya hadhira yake kwa namna ambayo yeye binafsi anaona kuwa ni sahihi kufanya hivyo. Basi, lengo la makala haya ni kubainisha matumizi ya mbinu ya weusi na ya uwili katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea ya Ken Walibora.
Isitoshe, makala haya yataeleza dhima ya weusi na uwili katika riwaya hii. Makala haya yametumikiza nadharia ya Elimumtindo kwa mtazamo wa Leech na Short (1981). Data ya makala ilipatikana maktabani
kwa kusoma riwaya teule kisha ikachanganuliwa kwa misingi ya nadharia iliyoteuliwa na lengo la makala. Ilibainika
kuwa mwandishi ametumia mbinu ya weusi ili kuashiria kukosa tumaini, matatizo ya wahusika, dhuluma dhidi ya Waafrika kutokakwa Wakoloni, hatari, kutoshughulikiwa,ukali, na pia tisho. Mtafiti alibaini kuwa sababu zilizomfanya mwandishi kutumia mbinu ya uwili ili kuashiria ubunifu na uhuru wake katika utunzi. Istilahi Muhimu: Weusi, Uwili, Elimumtindo.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Matumizi ya Mbinu ya Weusi na Uwili: Tathmini ya Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea (Dkt. Dorcas Muendi Musyimi Chuo Kikuu cha Chuka)”

Your email address will not be published. Required fields are marked *