Athari Za Vita Vya Ukabila: Tathmini Ya Chozi La Heri ( Dkt. Dorcas Muendi Musyimi Chuo Kikuu cha Chuka)

Sale!

KSh5,000.00

Category:

Description

IKISIRI
Nchini Kenya, kumekuwepo na vita vya wenyewe kwa wenyewe huku vikijikita katika misingi ya kikabila. Fasihi ni kioo cha
jamii na hali kadhalika ni chombo ambacho kinaweza kutumiwa katika kuangazia masuala halisi katika jamii. Makala haya
yanakusudia kubainisha jinsi mwandishi Assumpta Matei alivyoangazia athari zinazotokana na vita vya kikabila katika
riwaya ya Chozi la Heri. Makala haya yataongozwa na nadharia ya uhalisia iliyoasisiwa katika karne ya 19 na E. Goffman. Kulingana na nadharia hii, mwandishi husukumwa na nia ya kuusawiri uhalisia katika ukamilifu na wakati wake
maalum. Riwaya ya Chozi la Heri (Matei,2017) iliteuliwa kimakusudi kwa kuwa maudhui yake yanahusiana moja kwa moja
na mada ya makala haya.

Kazi hii ni muhimu katika kuthibitisha kuwa fasihi ina uwezo wa kuelimisha jamii juu ya athari zinazotokana na vita vya kikabila na hatimayekuihamasisha ili kuleta amani na mshikamano katika nchi. Data ilichanganuliwa kwa kufuata lengo la makala na misingi ya kinadharia. Imebainika wazi kuwa mwandishi ameangazia athari za vita vya kikabila ambazo ni; vifo, uharibifu wa mali ya umma, kusambaratika kwa familia, kuwepo kwa watoto wa mitaani, ulanguzi wa dawa za kulevya, ubakaji, ukosefu wa chakula na mahitaji mengine ya kimsingi

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Athari Za Vita Vya Ukabila: Tathmini Ya Chozi La Heri ( Dkt. Dorcas Muendi Musyimi Chuo Kikuu cha Chuka)”

Your email address will not be published. Required fields are marked *