Matumizi ya Mbinu ya Weusi na Uwili: Tathmini ya Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea

  • Home
  • Downloads
  • Matumizi ya Mbinu ya Weusi na Uwili: Tathmini ya Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea
[featured_image]
  • Version
  • Download 15
  • File Size 765.65 KB
  • File Count 1
  • Create Date September 29, 2022
  • Last Updated September 29, 2022

Matumizi ya Mbinu ya Weusi na Uwili: Tathmini ya Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea

Kulingana na Wamitila (2008), matumizi ya mtindo katika kazi za fasihi ndicho kipengele ambacho humtofautisha mtunzi mmoja na mwingine. Hii inatokana na ukweli kwamba kila mtunzi anao mtindo wake wa kuwasilisha jambo mbele ya hadhira yake kwa namna ambayo yeye binafsi anaona kuwa ni sahihi kufanya hivyo. Basi, lengo la makala haya ni kubainisha matumizi ya mbinu ya weusi na ya uwili katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea ya Ken Walibora. Isitoshe, makala haya yataeleza dhima ya weusi na uwili katika riwaya hii. Makala haya yametumikiza nadharia ya Elimumtindo kwa mtazamo wa Leech na Short (1981).

Data ya makala ilipatikana maktabani kwa kusoma riwaya teule kisha ikachanganuliwa kwa misingi ya nadharia iliyoteuliwa na lengo la makala. Ilibainika kuwa mwandishi ametumia mbinu ya weusi ili kuashiria kukosa tumaini, matatizo ya wahusika, dhuluma dhidi ya Waafrika kutoka kwa Wakoloni, hatari, kutoshughulikiwa, ukali, na pia tisho. Mtafiti alibaini kuwa sababu zilizomfanya mwandishi kutumia mbinu ya uwili ili kuashiria ubunifu na uhuru wake katika utunzi.

Istilahi Muhimu: Weusi, Uwili, Elimumtindo

Attached Files

FileAction
78-84 Education and Social Sciences - Dkt Dorcas Muendi Musyimi,.pdfDownload

Leave A Comment