Athari Za Vita Vya Ukabila: Tathmini Ya Chozi La Heri

  • Home
  • Downloads
  • Athari Za Vita Vya Ukabila: Tathmini Ya Chozi La Heri
[featured_image]
  • Version
  • Download 94
  • File Size 1.04 MB
  • File Count 1
  • Create Date September 29, 2022
  • Last Updated September 29, 2022

Athari Za Vita Vya Ukabila: Tathmini Ya Chozi La Heri

Nchini Kenya, kumekuwepo na vita vya wenyewe kwa wenyewe huku vikijikita katika misingi ya kikabila. Fasihi ni kioo cha jamii na hali kadhalika ni chombo ambacho kinaweza kutumiwa katika kuangazia masuala halisi katika jamii. Makala haya yanakusudia kubainisha jinsi mwandishi Assumpta Matei alivyoangazia athari zinazotokana na vita vya kikabila katika riwaya ya Chozi la Heri.

Makala haya yataongozwa na nadharia ya uhalisia iliyoasisiwa katika karne ya 19 na E. Goffman. Kulingana na nadharia hii, mwandishi husukumwa na nia ya kuusawiri uhalisia katika ukamilifu na wakati wake maalum. Riwaya ya Chozi la Heri (Matei, 2017) iliteuliwa kimakusudi kwa kuwa maudhui yake yanahusiana moja kwa moja na mada ya makala haya. Kazi hii ni muhimu katika kuthibitisha kuwa fasihi ina uwezo wa kuelimisha jamii juu ya athari zinazotokana na vita vya kikabila na hatimaye kuihamasisha ili kuleta amani na mshikamano katika nchi. Data ilichanganuliwa kwa kufuata lengo la makala na misingi ya kinadharia. Imebainika wazi kuwa mwandishi ameangazia athari za vita vya kikabila ambazo ni; vifo, uharibifu wa mali ya umma, kusambaratika kwa familia, kuwepo kwa watoto wa mitaani, ulanguzi wa dawa za kulevya, ubakaji, ukosefu wa chakula na mahitaji mengine ya kimsingi.

Istilahi Muhimu: Athari, Vita, Ukabila.

Attached Files

FileAction
71- 77 Education and Social Sciences - Dkt Dorcas Muendi Musyimi.pdfDownload

Leave A Comment